You are currently viewing 60 YEARS UHURU DAY

60 YEARS UHURU DAY

Sikukuu ya Uhuru ni shauku iliyojaa matumaini tele ya kujitawala kifikra, kijamii, kimipaka na kiuchumi. Ikaleta mtazamo wa pamoja kujituma na kushirikiana.

Umoja thabiti, ukawa ndio mtazamo wa kuitimiza shauku hiyo. Kilitumika kila kilichoonekana kinafaa kufikia shauku hiyo, hata kinyonge kikawa na nguvu kwa umoja huo.

Dec. 09, 1961, shauku ikafikiwa na kuleta matumaini mapya na mapinduzi makubwa ya Taifa imara na chapakazi lenye maendeleo makini ya kiuchumi yenye sekta bora ikiwemo sekta ya fedha.

Tunajivunia kuwa sehemu ya sekta hii ndani ya miaka 60, tulivu ya amani.

Tunaahidi kuendelea kuchochea ukuwaji wa uchumi wa taifa na familia kwa ujumla.

Tunaungana na watanzania wote katika kusherehekea sikukuu ya uhuru wa taifa letu.

Tuzidi kudumisha uhuru wetu, umoja na amani.

Kazi iendelee….

Tunajali Uchumi wa familia.
#60YaUhuru