Katika familia tunakutana na changamoto nyingi sana kama kushindwa kukata bima ya familia kwa wakati, kushindwa kulipa ada kwa wakati, kushindwa kulipa kodi kwa wakati.
Familia nyingi zimekuwa zikiteseka na changamoto ya kutunza na kugawanya vyema kipato kinachopatikana. Pesa inaisha haraka na kushindwa kukamilisha malengo, kushindwa kuhudumia familia na kufanya maendeleo kwa wakati.
Fahamu akaunti 4 tofauti zinazoweza kukusaidia kugawanya vyema kipato na kutengeneza uchumi bora na imara wa familia.
Kila familia inapaswa kuwa na mgawanyo wa akaunti 4 tofauti ili kuweza kuwa na uchumi bora na imara wakati wote.
Akaunti hii ni akaunti ya pamoja ambayo kila mmoja anapaswa kutoa fungu kutoka kwenye kipato binafsi mnachokubaliana kwa ajili ya mahitaji ya familia kama kulipa kodi, ada, chakula, mavazi, matibabu, n.k.
Hii ni akaunti muhimu sana kwenye familia inayolenga kutimiza malengo, mipango na kuilinda familia dhidi ya majanga yasiyotabirika kama ajali, magonjwa, vifo n.k.
Familia lazima iweke mipango ya maendeleo na kuchukua hatua kidogo kidogo. Akaunti hii itakusaidia kutunza pesa kukamilisha mipango ya familia bila stresi kama kukamilisha ujenzi, kufanya uwekezaji, kuanzisha na kutanua biashara n.k.
Ni muhimu sana kila mmoja kuwa na akaunti yake binafsi ambayo anaweza kutoa pesa wakati wowote kufanya chochote akipendacho bila kuhojiwa. Unaweza kumwagilia moyo upendavyo, kununua mahitaji binafsi na kuanzisha mambo yako binafsi kutoka kwenye akaunti hii.
Tunajivunia sana kuwahudumia wateja wetu wapendwa kwa weledi, upendo, na kwa furaha. Tunawathamini sana wateja wetu kuendelea kufurahia huduma bora zenye nafuu kutoka Uchumi Bank
Hakika najivunia sana benki hii hasa kwa namna ya pekee inavyojali uchumi wa familia zenye kipato kidogo. Nimejiunga na benki hii tangu 2016, akaunti zenye faida zimenisaidia sana kutimiza malengo yangu ya kulipa ada ya watoto wetu kwa wakati. Endeleeni kukitunza chombo hiki.
Hii ndio benki yangu pendwa kabisa ninayojivunia wakati wote. Nimekuwa nikivuna na akaunti ya mavuno kila miezi mitatu hasa nikitunza pesa kwa malengo binafsi na familia yangu. Kwa kweli mnenisaidia sana mbinu za kutunza pesa na kuhakikisha nafikia malengo yangu kwa wakati kila mara. Mzidi kubarikiwa sana tena sana.